Header Ads

Header ADS

SWALAH SEHEMU YA SITA

 

*Assalaam Alaykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*

Tunaendelea na darasa letu la Swalah na tutaona ni Jinsi gani ya kuweka Mikono juu ya Kifua

                     *KUWEKA*
                      *MIKONO*
💠            *JUU YA KIFUA*         💠
       ```SEHEMU  YA  SITA```
============♦============

Mtume (صل الله عليه وسلم) *"Alikuwa akiweka mkono wa kulia nyuma ya kitanga cha mkono wa kushoto, kiwiko na kigasha*"  na aliwaamrisha Maswahaba wake kufanya hivyo"  na (mara nyingine) *"akiushika mkono wa kushoto kwa mkono wake wa kulia*" [( An-Nasaaiy na Darqutiny )]

*"Alikuwa akiiweka juu ya kifua chake"* [( Abu Dawuud na Ibni Khuzaymah )]

Pia, alikuwa akikataza mtu kuweka mkono juu ya kiuno wakati wa Swalah na aliweka mkono wake juu ya kiuno (kuonyesha makosa hayo). Na hii ndio swilb aliyokuwa akikataza.[(

*Tanbihi*
Kuiweka katika kifua ndivyo ilivyothibiti katika Sunnah, na kinyume chake ni aidha dhaifu au haina msingi.

          *KUTAZAMA MAHALI*
              *PA KUSUJUDU*
                *NA KUSHUU*
💠       *(UNYENYEKEVU)*         💠
============♦===========.
"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiinamisha kichwa chake wakati wa Swalah na kukongomeza (kuyaelekeza) macho yake katika ardhi
"Alipoingia katika Kaabah, hakuacha jicho lake kutazama sehemu ya kusujudu hadi alipotoka nje"  na alisema:- *((Haipasi kuweko na kitu chochote katika Nyumba kitakachomshawishi mwenye kuswali))*"[(Abu Dawuud na Ahmad)]

*"Alikuwa akikataza kuinua macho kutazama mbinguni"* [( Al Bukhaariy na Abu Daawuud )] na alishikilia makatazo haya sana hadi alisema: *((Watu lazima waache kutazama juu mbinguni katika Swalah au macho yao hayatorudi kwao))* [na katika riwaaya nyingine] *((…au macho yao yatapofushwa))*[( Al Bukhaariy, Muslim na Siraaj )]

Katika Hadiyth nyingine: *((Mnaposwali msiangaze huku na kule kwani ALLAAH Huelekeza Uso Wake mbele ya uso wa mja Wake madamu mja hatoangaza kwengine))*.[ ( At-Tirmidhiy na Al Haakim)] Akasema pia kuhusu kuangaza huku na kule: *((Ni kunyakuliwa ambako Shaytwaan hunyakuwa katika Swalah ya mja anaposwali))* [( Bukhariy na Abu Daawuud )]

Akasema pia (صلى الله عليه وآله وسلم): *((ALLAAH Haachi kuelekea kwa mja katika Swalah madamu tu mja haangazi huku na kule, anapogeuza uso wake mbali, ALLAAH Hugeuka mbali naye))* na *"Akakataza mambo matatu; kudonoa kama jogoo, kuchutama kama mbawa na kuangaza kama fisi"* , vile vile alikuwa akisema: *((Swalini Swalah ya kuaga (dunia) kama kwamba mnamuona Yeye (ALLAAH ) na kama hamumuoni, hakika Yeye Anakuoneni))*, na (akisema), *((Mtu yeyote anayefikwa na Swalah ya fardhi akatawadha vizuri, akakamilisha khushuu (unyenyekevu) zake, na rukuu zake, hakika itakuwa ni kafara ya dhambi alizotenda kabla ya Swalah hiyo madamu hajatenda dhambi kubwa, hali hiyo ni kwa mwaka wote))* [( Muslim)]

Mara moja yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali katika khamiysah *[ nguo ya Sufi iliyo na alama)]* (na alipokuwa akiswali) alizitazama alama zake. Alipomaliza akasema: *((Ipelekeeni khamiysah hii yangu kwa Abu Jahm na nileteeni (badala yake) anbijaaniyyah[ nguo ya kukwaruza isiyo na alama)] kwani imenipotezea umakini wangu katika Swalah))* [katika usimulizi mmoja] *((…kwani nimetazama alama zake wakati wa Swalah ilikaribia kunitia katika mtihani))*[( Bukhariy na Muslim)]

Pia Mama wa Waumini 'Aaishah (رضي الله عنها) alikuwa na kitambaa cha picha kilichotandazwa mbele ya sahwah  ambayo Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali mbele yake, akasema: *((Iondoshelee mbali, [kwani picha zake hazikuacha kunishawishi katika Swalah]))*[ Bukhariy, Muslim na Abu A'waanah ]
Alikuwa akisema pia: *((Hakuna kuswali chakula kinapokuwa tayari, wala mtu anapotaka kukidhi haja kubwa na ndogo))*[( Bukhariy na Muslim)]

In Shaa ALLAAH tutaendelea tena

*RAUDHWATUL ILM*

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 

No comments

Powered by Blogger.