Header Ads

Header ADS

SWALAH SEHEMU YA 12

 *Assalaam Alaykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*


Tunaendelea na darasa letu la Swalah 



                *KISOMO CHAKE*

                  *(صلى الله عليه وآله وسلم)*

💠  *BAADA YA AL-FAATIHAH*  💠

  ```SEHEMU YA KUMI NA MBILI```

============♦===========

*KISOMO CHAKE (صلى الله عليه وآله وسلم) BAADA YA AL-FAATIHAH*

 

Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surah nyingine baada ya al-Faatihah, na alikuwa akikirefusha hicho kisomo mara nyingine, na mara nyingine akikifupisha kwa sababu ya safari, au kikohozi, au maradhi au kilio cha mtoto.

 

Kama alivyosema Anas Ibn Maalik (رضي الله عنه): *"Alifupisha  Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) siku moja katika Swalah ya Alfajiri"* (Na Katika Hadiyth nyingine, *"Aliswali (صلى الله عليه وآله وسلم) Swalah ya Asubuhi akasoma Surah mbili zilizo fupi sana katika Qur-aan)*". Pakaulizwa: *"Ewe Mjumbe wa ALLAAH, kwa nini umefupisha?"* Akasema: *((Nimesikia kilio cha mtoto hivyo nimehisi kwamba mama yake yu pamoja na sisi anaswali, kwa hiyo nikataka kumpa wasaa mama yake kwa ajili yake))* [( Ahmad kwa isnaad Swahiyh )]

 

Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: *((Hakika mimi huingia katika Swalah hali ya kuwa ninataka kuirefusha, ninaposikia kilio cha mtoto, hufupisha Swalah yangu kwa kuelewa machungu makubwa ya mama yake kwa kilio chake))*[( Al-Bukhaariy Na Muslim )]

 

*"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akianza kusoma kutoka mwanzo wa Surah, na aghlabu huimaliza"*

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: *((Ipeni kila Surah sehemu yake katika Rukuu na Sujuud))*[( Ibn Abi Shaybah (1/100/1), Ahmad na 'Abdul-Ghaniy Al-Maqdisiy katika Sunan (9/2) kwa isnaad Swahiyh. 

 

Katika usemi mwengine: *((Kwa Kila Surah Raka’ah))* [{ Ibn Naswr na At-Twahaawiy kwa isnaad Swahiyh }] 

 

Mara nyingine huigawa Surah katika Rakaa mbili na mara nyingine huirudia yote nzima katika Raka’ah ya pili.

 

Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiunganisha katika Rakaah baina  Surah mbili au zaidi.

 

Mtu Mmoja katika Answaar alikuwa akiswalisha katika Msikiti wa Qubaa, na alikuwa kila anapoanza kuwasomea Surah katika Swalah baada ya al-Faatihah, huanza kwa ‘Qul Huwa Llaahu Ahad’ [Suratul-Ikhlaasw: 112 ] hadi mwisho, kisha anasoma Surah nyingine pamoja nayo, na alikuwa akifanya hivyo katika kila Raka’ah. wenzake walimuuliza kwa kusema: *"Unaanza na Surah hii, kisha huoni kama inakutosheleza mpaka unasoma nyingine, basi chagua moja; isome hiyo pekee au iache na uisome nyingine"*. Akasema: *"Sitoiacha, ikiwa mtapenda mimi nikuswalisheni (niwe Imaam wenu) kwayo, nitaendelea, lakini ikiwa mtachukiwa, sitokuswalisheni tena"*, na walikuwa wakimuona kuwa yeye ni mbora miongoni mwao, na pia hawakuwa wanapendekezewa kuswalishwa na mwenginewe. Na pindi alipokuja Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamuelezea habari hiyo, Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): *((Ewe fulani, kipi kinachokuzuia kutekeleza wanayokuomba watu wako? Na Kipi kinachokupelekea kuwa lazima uisome Surah hii katika kila Raka’ah?))* Akasema: *"Hakika Naipenda Surah hii"* akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): *((Mapenzi yako kwayo yatakuingiza Peponi))* [ ( Muslim )]

 

 

 In Shaa ALLAAH tutaendelea tena biidhiniLLAAHI. 


*+97433799776*


QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.