SWALAH SEHEMU YA 13
*Assalaam Alaykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*
*KUCHANGANYA KWAKE*
*(صلى الله عليه وآله وسلم)*
*BAINA YA SURAH*
*ZINAZOFANANA NA*
💠 *NYINGINEZO KATIKA RAKAA*💠
```SEHEMU YA KUMI NA TATU```
============="♦============
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiunganisha baina ya An-Nadhwaair (( *"An-Nadhwaair*":-- Ni Surah zilizofanana katika maana. Ni kama zile ambazo zote zina nasaha, maamrisho au visa.)]
miongoni mwa Surah za Mufasswal ([ *Mufasswal*, hizi zimekubalika kuwa zinazomalizia Qur-aan mwisho, na mwanzo wake ni Surat Qaaf (Namba 50) kwa rai iliyo sahihi zaidi ]), hivyo basi alikuwa akisoma jozi mojawapo za Surah zifuatazo katika Rakaa moja ([ Al-Bukhaary na Muslim )]
Ar-Rahmaan (55: 78) ([4]) na An-Najm (53: 62).
Al-Qamar (54: 55) na Al-Haaqqah (69: 52).
At-Twuur (52: 49) na Adh-Dhaariyaat (51: 60).
Al-Waaqi'ah (56: 96) na Al-Qalam (68: 52).
Al-Ma'arij (70:44) na An-Naazi'aat (79:46).
Al-Mutwaffifiyn (83: 36) na 'Abasa (80: 42).
Al-Muddaththir (74: 56) na Al-Muzzammil (73: 20).
Ad-Dahr (76: 31) na Al-Qiyaamah (75: 40).
An-Nabaa (78: 40) na Al-Mursalaat (77: 50).
Ad-Dukhaan (44: 59) na At-Takwiyr (81: 29).
Mara nyingine alikuwa akiunganisha baina ya Surah kutoka Sab'at-Twiwaal (Surah Saba ndefu); kama al-Baqarah, an-Nisaa na aal-'Imraan katika Rakaa moja kwenye Swalah ya usiku kama itakavyokuja. Na alikuwa akisema:
*((Swalah bora kabisa ni yenye kisimamo kirefu)).*
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anaposoma:-
*((أَلَيْسَ ذَلِكَ بِقَادِرٍ عَلَى أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَى))*
Alaysa dhaalika biqaadirin ‘alaa-an Yuhyiyal Mawtaa
*((Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu))*. [Al-Qiyaamah 75: 40)
Husema:
" *Sub-haanak fabalaa* "
Utukufu ni Wako Ndio hapana shaka
Na anaposoma:-
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى
Sabb-hisma Rabbikal A’laa
*((Litakase Jina la Mola wako Mlezi Aliye juu kabisa))*. [Al-A'laa 87: 1)
Husema:
*Sub-haana Rabbiyal A’laa*
Ametakasika Mola wangu Aliye juu.
In Shaa ALLAAH tutaendelea tena .
*+97433799776*
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments