SWALAH SEHEMU YA 14
*Assalaam A'laykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*
*RUHUSA YA KUSOMA*
💠 *AL-FAATIHAH PEKEE* 💠
```SEHEMU YA 14```
=============♦===========.
Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه) alikuwa akiswali 'Ishaa (ya mwisho) pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha akirudi huwaswalisha wenzake. Usiku mmoja, aliporudi aliwaswalisha, na akaswali kijana mmoja katika watu wake [wa Banu Salamah aliyeitwa Sulaym], lakini (Swalah) ilipokuwa ndefu kwa yule kijana, [alijiondokea] na akaswali [pembezoni mwa Msikiti]. Kisha akatoka na kushika ungwe za ngamia wake na akajiondokea.
Mu'aadh (رضي الله عنه) Alipomaliza kuswali alielezwa yaliyotokea, akasema: *"Bila shaka ana baadhi ya unafiki!* *Nitamweleza Mjumbe wa ALLAAH (صلى الله عليه وآله وسلم) alivyofanya"*.
Na yule kijana naye akasema: *"Nami nitamweleza Mjumbe wa ALLAAH (صلى الله عليه وآله وسلم) alivyofanya"*.
Kulipopambazuka, walikuja kwa Mjumbe wa ALLAAH (صلى الله عليه وآله وسلم), basi Mu'aadh akamweleza yale aliyoyafanya yule kijana. Kijana akasema: *"Ewe Mjumbe wa ALLAAH ! Yeye hukaa na wewe muda mrefu, kisha anarudi na kuturefushia"*. Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: *((Je, wewe ni mfitini ewe Mu'aadh?!))*.
Na akasema kumwambia yule kijana: *((Vipi unafanya unaposwali ewe mtoto wa ndugu yangu?))* Akamjibu: *"Nasoma Kifungulio cha Kitabu, kisha namuomba ALLAAH Pepo, na najikinga Kwake kutokana na moto. Na hakika mimi sielewi dandanah([ *"Dandanah" ni mtu anaposema maneno kwa madaha na kusikiwa mvumo wa maneno yake lakini hayafahamiki. Ni karibu kidogo na kunong'ona. (An-Nihaayah)])* yako wala dandanah ya Mu'aadh!" Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: *((Hakika Mimi na Mu'aadh tuko katika hayo hayo mambo mawili, au mfano wake))*. Msimulizi alisema: "Yule Kijana akasema: *"Lakini Mu'aadh ataelewa watakapokuja watu wakapewa habari kwamba adui wamefika"*. Msimulizi akasema: *"(Hivyo) Adui wakaja na yule kijana akafa shahidi.* Baada ya hapo, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema kumwambia Mu'aadh: *((Amefanya nini yule aliyejadiliana nami na wewe?))*. Akasema: *"Ewe Mjumbe wa ALLAAH ! Amemsadikisha ALLAAH , nami sikuwa mkweli, amekufa shahidi*".([ Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1634)])
In shaa ALLAAH tutaendelea tena biidhiniLLAAHI.
*+97433799776*
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments