Header Ads

Header ADS

SWALAH SEHEMU YA 15

 *Assalaam A'laykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*




               *KUNYANYUA SAUTI* 

                     *NA KUSOMA*

         *KISOMO CHA KIMYA KIMYA* 

             *KATIKA SWALAH TANO*

                               *NA* 

                      *NYINGINEZO*

💠```SEHEMU YA KUMI NA TANO``` 💠

=============♦============. 

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitoa sauti katika Swalah ya Asubuhi na katika Rakaa mbili za mwanzo za Swalah ya Magharibi na 'Ishaa, na akisoma kimya kimya katika Swalah za Adhuhuri, Alasiri na Rakaa ya tatu ya Swalah ya Magharibi na Rakaa mbili za mwisho za Swalah ya 'Ishaa.([ An Nawaawiy ])

 

Walikuwa wakiweza kuelewa kuwa anasoma kimya kimya kutokana na mtikisiko wa ndevu zake na kwa kuwasikilizisha Aayah mara nyingine ([ Al Bukhariy na Muslim ]).

 

Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitoa sauti katika Swalah ya Ijumaa na Swalah za 'Iyd mbili, na Swalah ya kuomba mvua, na Swalah ya kupatwa jua au mwezi.

 

 

 

             *KUNYANYUA SAUTI* 

                               *NA* 

                  *KUSOMA KIMYA* 

       *KATIKA SWALAH YA USIKU*

=============♦=============

 

Ama katika Swalah ya usiku, mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma kimya kimya na mara nyingine kwa sauti, na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anaposoma hali ya kuwa yuko nyumbani kwake, humsikia kisomo chake aliyeko barazani mwake ([ *Abu Daawuud na At-Tirmidhiy katika Shamaail ikiwa na isnaad nzuri. Hadiyth ina maana kwamba yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa yu katikati baina ya ukimya na kupaza sauti*. ]).

 

Huenda mara moja moja akapandisha sauti yake zaidi ya hivyo hadi akaisikia aliyelala([ An-Nassaaiy ]).  (Yaani nje ya baraza/uwa).

 

Na hivyo ndivyo alivyowaamrisha Abu Bakr na 'Umar (رضي الله عنهم) wakati alipokuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) ametoka nje usiku mmoja akatahamaki kumuona Abu Bakr (رضي الله عنه) anaswali huku akiishusha sauti yake chini. Na akampitia ‘Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) aliyekuwa akiswali kwa kunyanyua sauti yake juu. (Baadaye,) walipokutana pamoja kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: *((Ewe Abu Bakr! Nilikupitia na hali ukiwa unaswali kwa kushusha sauti yako))*. Akasema: *"Nimemsikilizisha niliyekuwa nanong’ona Naye ewe Mjumbe wa ALLAAH "*.  Akamwambia 'Umar: *((Nilikupitia na hali ukiwa unaswali kwa kupaza sauti yako)).* Akasema: *"Ewe Mjumbe wa ALLAAH ! Nilikuwa naondosha usingizi na namkimbiza Shaytwaan*". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: *((Ewe Abu Bakr! Pandisha sauti yako kidogo*. Na akasema kumwambia 'Umar: *((Ewe 'Umar! punguza sauti yako kidogo))*([ Abu Daawuud na Al-Haakim ]).

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema:- *((Mwenye kusoma Qur-aan kwa kunyanyua sauti, ni kama mfano wa mwenye kutoa sadaka kwa kuonekana na watu, na mwenye kusoma Qur-aan kimya kimya kwa kushusha sauti yake, ni kama mwenye kutoa sadaka kwa siri))*. 

 

In shaa ALLAAH tutaendelea tena biidhiniLLAAHI 


*+97433799776*



QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.