Header Ads

Header ADS

SWALAH SEHEMU YA KUMI

 

A'ssalam alaykum Wa Rahamatullaah Wa Barakatuh

*KUFUTWA KISOMO*
               *NYUMA YA IMAAM*
   *KATIKA SWALAH ZA JAHRIYYAH*
  *(SWALAH ZA KUNYANYUA SAUTI)* 
💠```SEHEMU YA KUMI```💠
============♦============.
Alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ameruhusu kwa wale waliokuwa ma-amuma kuisoma Suratul-Faatihah nyuma ya Imaam katika Swalah za jahriyyah, na mara moja alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم), *"Akiswali Alfajiri na kisomo kikawa kigumu kwake.* Alipomaliza alisema: *((Labda mnasoma nyuma ya Imaam wenu!))*. Tukasema: *"Ndio hadhdhan, Ewe Mjumbe wa ALLAAH "*. Akasema: *((Basi Msifanye hivyo isipokuwa [kwa kusoma mmoja wenu] Ufunguo wa Kitabu, kwani hakuna Swalah kwa asiyeisoma))*[( Al Bukhariy )]

Kisha aliwakataza kusoma katika Swalah za *jahriyyah* kabisa, na hilo lilitokea wakati,

"Alipomaliza Swalah ambayo alikuwa akisoma kwa sauti [katika usimulizi (mmoja) ilikuwa Swalah ya Alfajiri] basi akauliza: *((Je, kuna (yeyote) aliyekuwa akisoma pamoja nami hivi sasa?))* Mtu mmoja akajibu: *"Ndio, mimi Ewe Mjumbe wa ALLAAH*". Akasema: *((Mimi Nasema: sasa kwa nini naingiliwa kati katika kisomo changu]* [Abu Hurayrah alisema]: (Hivyo) watu wakaacha kusoma pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kila anapokuwa anasoma kwa sauti baada ya kusikia hivyo kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) [wakawa wanaendelea kusoma kimya kimya kila anapokuwa Imaam haisomi kwa sauti] [( Maalik, Humaydy, Al-Bukhaariy)]

Pia Akaufanya (صلى الله عليه وآله وسلم) ukimya katika kisomo cha Imaam kuwa ni sehemu katika kukamilisha kumfuata Imaam, kwa kusema: *((Kwa hakika amewekwa Imaam ili apatwe kufuatwa, hivyo anapoleta takbiyr, na nyinyi leteni takbiyr, na anaposoma kaeni kimya))*, kama alivyofanya kumsikiliza Imaam kuwa kunatosheleza na kisomo nyuma yake, kwa kusema (aliposema): ((Mwenye kuwa na Imaam, basi kisomo cha Imaam huyo ni kisomo chake)). Hii inahusu Swalah za jahriyyah.



           *KUWAJIBIKA KUSOMA*
*KATIKA SWALAH ZA SIRRIYYAH*
             *(SWALAH ZA KIMYA)*
=============♦============
Ama katika Swalah za kimya kimya, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaachilia waendelea kusoma humo. Jaabir alisema: *"Tulikuwa tukisoma katika (Swalah ya) Adhuhuri na 'Aswr nyuma ya Imaam katika Rakaa mbili za mwanzo Suratul-Faatihah na Surah nyingine, na katika mbili za mwisho Suratul-Faatihah*[( Ibn Maajah)]

Lakini, alichukizwa kwa tashwishi na kubabaishwa, kwa kisomo chao pale aliposwali Adhuhuri na Maswahaba akauliza: *((Nani katika nyinyi aliyesoma: "Sabbihisma Rabbikal A’laa" [Suratul-A'laa, 87:1]))*. Mtu mmoja akajibu: *"ni mimi" [sikuwa na kusudio lo lote lile kwa kuisoma ila kheri]* Akasema: *((Nilijua kuwa kuna mtu anavutana na mimi kwayo))*[( Muslim, Abu 'Awaanah na Siraaj )]

Na Katika Hadiyth nyingine: *"Walikuwa wakisoma nyuma ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), hivyo akasema: ((Mmenibabaisha katika kisomo changu))*[( Al-Bukhaariy katika makala yake, Ahmad na Siraaj kwa isnaad nzuri.)]

Akasema: *((Anayeswali huwa ananongo’na na Mola wake, basi aangalie cha kumnongo’neza, wala msisome Qur-aan pamoja wote kwa sauti))*[ ( Maalik na al-Bukhaariy katika Af'aal al-'Ibaad kwa isnaad Swahiyh.)]

Pia alikuwa akisema: *((Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha ALLAAH atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, (wala) sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi moja))* [(At-Trimidhiy na Ibn Maajah kwa isnaad Swahiyh.)]

*Tanbihi*
========.
Katika rai Zote juu ya kusoma *Maamuma* nyuma ya Imaam katika Swalah ya *Jahriyyah* ( Ya Sauti ) ni yenye nguvu na  ni Kusoma Suratul Faatihah tu kwa Sauti ya chini ya kujisikia yeye mwenyewe bila kumchanganga Imaam na aliyekuwa pembeni yako na kutulia kumsikiliza Imaam akiendelea kusoma Surah ingine baada ya Suratul Faatihah.

Na katika Swalah ya *Sirriyyah* ( Ya Kimya ) Maamuma atasoma nyuma ya Imaam atasoma Suratul Faatihah na Surah ingine katika rakaa' mbili za Mwanzo Kama ilivyozoeleka kwa sauti ya kujiskia yeye Mwenyewe na katika rakaa mbili zingine atasoma Surah tul Faatihah tu

In shaa Allah tunaendelea

*+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
📗〽〽〽〽〽〽〽〽〽📗

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 

No comments

Powered by Blogger.