Header Ads

Header ADS

SWALAH SEHEMU YA TISA



*Assalaam A'laykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*

Tunaendelea na darasa letu la Swalah Jana tuliona Jinsi Mtume ( صل الله عليه وسلم ) alivyokuwa akiisoma Suratul Faatihah yaani Kituo kwa Kituo. Na Leo tunaona ulazima Wa Suratul Faatihah.

                    *ULAZIMA*
                           *WA*
     *KUSOMA SURATUL FAATIHAH*
                            *NA*
💠         *FADHILA ZAKE*           💠
                ```SEHEMU YA TISA```
============♦===========. 

Alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akitilia mkazo na kusisitiza kuhusiana na (Alisisitiza mno) umuhimu wa Surah hii, alikuwa akisema: *((Hakuna Swalah kwa asiyesoma [ndani yake] Ufunguo wa Kitabu))*
[( Al-Bukhaairy, Muslim, Abu 'Awaanah na Al-Bayhaqiy. Imetolewa katika Al-Irwaa (302) ]

Na Katika usemi mwengine: *((Swalah haitimii mtu asiposoma ndani yake Ufunguo wa Kitabu))*
[( Ad-Daaraqutwniy)]

*Na wakati mengine anasema*:-  ((Mwenye kuswali Swalah yeyote ile bila ya kusoma ndani yake Ufunguo wa Kitabu basi hiyo Swalah ni khiddaaj  [( *Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alifasiri kwa kusema haikutimilia*)] , ni *khiddaaj*, ni *khiddaaj*, haikukamilika))
[( *Muslim na Abu 'Awaanah*]


Na anasema (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa:-

ALLAAH (سبحانه وتعالى) Amesema: *"Nimegawa Swalah baina Yangu na mja Wangu (katika) sehemu mbili; nusu ya kwanza ni Yangu na nusu nyengine iliyobaki ni ya mja Wangu, na mja Wangu atapata alichokiomba"*

(Kisha) Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema:- Someni: Mja anasema: *"Al-hamdu Llillaahi Rabbil ‘Alaamiyn”*, ALLAAH (سبحانه وتعالى) Husema *"Mja Wangu amenisifu*" Mja akisema: *"Ar-Rahmaanir Rahiym*”, ALLAAH Husema: *"Mja Wangu amenitukuza*" Mja akisema: *"Maalik/Malik*”, ALLAAH Husema: *Mja Wangu Ameniadhimisha"* Mja akisema: *"Iyyaaka na’budu wa iyyaaka nasta’iyn”*, [Husema]: *"Hii ni baina Yangu na Mja Wangu, na Mja wangu atapata atachoomba"*. Mja akisema: *"Ih-dinaas swiraattal mustaqiym, swiraattal Laadhiyna An’amta ‘alayhim ghayril maghdhuubi ‘alayhim wala-dhwaaliyn”,* [Husema] Yote haya ni ya Mja Wangu na Mja Wangu atapata aliyoyaomba"
[( *Muslim, Abu 'Awaanah na Maalik* )]

Alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: *((ALLAAH Aliyetukuka hakuteremsha katika Tawraat wala katika Injiyl chochote kile chenye kufanana na Ummul Qur-aan -Mama wa Qur-aan-, nayo Ni Aayah Saba zisomwazo mara kwa mara [Na Qur-aan Tukufu niliyopewa])*[( An-Nassaiy na Al-Haakim)]


Alimuamrisha (صلى الله عليه وآله وسلم) *"Mtu aliyeswali vibaya" aisome hiyo Faatihatul Kitaabu katika Swalah yake"* (Lakini) na kwa yule asiyeweza kuihifadhi alimuambia (aliyeisahau): Sema:- *Subhaana Llaah, Wal-Hamdu Lillaah, wala ilaaha illa Llaahu, wa ALLAAHU Akbar, wala Hawla wala Quwwata ila bi Llaah*

✳ Maana yake
*"Ametakasika ALLAAH  na sifa njema ni za ALLAAH  na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ALLAAH , na ALLAAH  ni Mkubwa na Hakuna uwezo wala nguvu ila za ALLAAH*" [(Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/80/2), Al-Haakim, At-Twabaraaniy na Ibn Hibbaan ambae pamoja na Al-Haakim, wamesema ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana nayo. Imo katika Al-Irwaa (303) )]


Na (Pia) alimuambia *"aliyeswali kimakosa":*- *((Ikiwa umehifadhi cho chote kile katika Qur-aan basi isome, vyenginevyo msifu ALLAAH , kiri Ukubwa Wake, na kiri kwamba hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye))*[( Abu Daawuud na At-Tirmidhiy ambae amesema ni nzuri; isnaad yake ni Swahiyh. (Swahiyh Abu Daawuud Namba. 807)]

In Shaa ALLAAH tutaendelea tena

*+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
📗〽〽〽〽〽〽〽〽〽📗

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 

 

No comments

Powered by Blogger.