TABIA NJEMA SEHEMU YA 10
🌹 *_رياض الصالحين (SEH:10)_* 🌹
🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
🔻 _*MAHIMIZO YA KUZIDISHA KUTENDA KHERI MWISHO WA UMRI*_🔻
inampasa mtu kila umri wake ukisogea basi afanye bidii yakuzidisha kufanya mambo ya kheri
Pia vijana nao hawapaswi kuwa nyuma : Bali wakithirishe kufanya ibada kwani mtu hajui lini atafariki
Wema ni ule ambao unamalizikia nao : mtu usijifaharishe kwa wema wako wa zamani
Wala usijidharau kwa uovu wako wa sasa : Pia mtu hatakiwi avunjike moyo kutokana na makosa ambayo alikuwa akiyafanya hapo awali kwani mtume ﷺ anasema kuwa :
Huenda mtu akafanya matendo ya watu wa peponi mpaka ikabakia baina yake na pepo ni dhiraa tu lakini baadae akafanya matendo ya watu wa motoni nae akaingizwa humo
Napia huenda mtu akafanya matendo ya watu wa motoni ikawa yeye na moto ime bakia dhiraa tu lakini baadae akafanya matendo ya watu wa peponi akainhizwa humo
👉 Kwaio inampasa mwanaadamu kadri umri wake unavyokuwa basi ajitahid kufanya matendo mema : kwani mtume amesema :
*_Allah hakumbakishia udhuru mtu aliemuakhirishia { aliemchelewesha } mauti yake hata akafika umri wa miaka sitini_* { bukhari : 4970 }
👉 Kwaio kadri mtu umri unavyosogea anatakiwa awe anajua mambo yote ya kisheria ambayo ni wajibu kwake
Mfano :
1) akitaka kutia udhu ajue vipi mtu anatakiwa atawadhe
2) akitaka kuswali ajue swala inaswaliwa vipi
3) akitaka kufunga ajue vipi mtu anatakiwa afunge na mambo gani yanabatilisha funga
{ sharhu riyadhu swalihina : 1/381 }
👉. Kwaio kadri unavyokuwa mkubwa hua huna udhuru tena wakwenda kumueleza mola wako kuwa hajakupa mda ukapata kufanya ibada au kusoma dini yako : Kwaio ni wajibu mwanaadamu ajifunze dini yake.
lakini pia katika Tabia njema tunajifunza kuwa
Ikiwa wewe Allah amekuokoa na kufanya dhambi Fulani :
Mfano zamani ulikuwa unapenda nyimbo , Kutwaaa disko
Au Kutwaaa ulevi au uzinifu
Leo Allah amekujaalia kuiona Nuru na umeifuata haki 👈 usianze kujikweza ukajiona wewe ni wa peponi na wale ni wa motoni
👆Bali kwanza umshukuru Allah kwa kukuokoa wewe , pia ufanye ijtihada yakuwanasihi wale wote wafanyao uovu Huo ili waachane nao huenda Allah nao akawafumbua macho
Nasio kuanza kuwa ingiza watu motoni kisa tu wewe lile jambo Allah amekuepusha nalo kwani huwezi jua Allah amewakadiria nin na huenda mwisho wa uhai wao Allah nao akawaongoa
Kwaio unapoona MTU anafanya jambo Sio sahihi basi nikujitahidi kuweza kumfahamisha na kumnasihi.
_________
Itaendelea In Shaa Allah
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments