Header Ads

Header ADS

TABIA NJEMA SEHEMU YA 9

 

🌹 *_رياض الصالحين(SEH:9)_*  🌹

🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂

🔻 *_KUWA MKWELI_* 🔻

→ Uislamu unatuhimiza kushikamana na ukweli : na ukweli umegawika sehemu kuu mbili

*_Katika Maneno/ kauli_*

→ hapa muislamu anatakiwa kuzungumza ukweli au Habari ambazo zimetokea kweli

*_Ukweli katika vitendo_*

→ Hapa muislamu anatakiwa undani wake uwe sawa na udhahiri wake : yani kama unafanya jambo liwe linawafikiana na yalio moyoni mwako

a} Mwenye kufanya riya Sio mkweli kwani huwaonesha watu kuwa yeye ni mcha mungu wakati hayupo hivyo

b} Anaemshirikisha Allah sie mkweli kwani huonesha watu anamuabudu / kumtegemea Allah kumbe anategemea mizimwi , mashetani au waganga wake

c} Mnafiki nae sie mkweli kwani hudhihirisha imani wakati hayupo hivyo moyoni

d} mzushi / mtu wa bidaaa pia nae sie mkweli kwani huonesha anampenda na kumfuata mtume ﷺ kumbe kinyume chake anafanya yale ambayo wala mtume wa Allah hajafundisha

📚 شرح رياض الصالحين { ١/١٣٨ }
____

Zimekuja dalili mbali mbali katika Quran na sunna kututaka tushikamane na Tabia ya kuwa wakweli kama ifuatavyo :

(❶) " Enyi mlio amini! Mcheni Allah, na kuweni pamoja na wakweli  " { 9:119 }

(❷) " Ut'iifu na kauli njema. Na jambo likisha azimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa Allah, bila ya shaka itakuwa ni kheri kwao. " { 47: 21 }

🔻 *_MAENEO AMBAYO TUMEKITHIRI KUWA WAONGO_* 🔻

➊ Kuandaa makala / post za uongo ili kuwafurahisha watu au kuwachafua watu

➋ kusema uongo hadi kuapa ili kula mali za watu kwa Dhulma

→ mtu anaweza akakuapia : wallahi ninashida nisaidie , au sijala leo yapili , au mtu anasema uongo na kufoji nyaraka ili adhulumu ardhi au nyumba ya mwenziwe

➌ katika kufanya biashara :

→ mtu anaweza kusema uongo hii ni Mpya , Asali hii ni oriji , maziwa haya hayana maji , simu hii inakaa chaji siku tatu nk ili tu apate kuuza biashara zake

👆hayo yote hayatakiwi kwa muislamu Bali Tunapaswa kushikamana na ukweli

Itaendelea In Shaa Allah

_*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*_

https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A


📚📚

  📚

🌹 _*NYONGEZA*_🌹

Hapa wafanya biashara tunatakiwa tuwe makini sanaaa

Na Allah hayupo msikitini tu pekee mali Tunapaswa kufuata maamrisho na kuacha makatazo yake katika nyanja zetu zote za kimaisha

1) hutakiwi uchanganye mchele : mbeya na mchele wa ajabu ajabu

Halafu mtu akija unamwambia hii mbeya safi kabisa ukipika nyumba ya 3 Wana sikia harufu

→ kama umeamua kuchanganya basi akija mtu mwambia kuwa huu nimeuchanganya Kwaio anahiari achukue au aache

2) kama una uza Asali : Sio unatengeneza sukari Halafu unawaambia watu hii Asali oriji kutoka Pemba : kumbe sukari umefanya mambo yako Halafu unadanganya watu

3) kama simu yako ushaichoka unataka  kuiuza basi Mwambie mtu ukweli kuwa hii inakaa chaji nusu Saaa , au ukiongea mtu humsikii uzuri

Sio unamwambia hii Mpya ime tumika mwezi mmoja tu

3) wauzaji matunda katika kupanga Sio chini mnaweka mabaya au mabovu kisha juu mnaweka mazuri ili kuvutia watu

Mtu bora umwambie kuwa kuna mengine yashaanza kuvurugika nk.

Kutokana na Tabia za waislamu sisi kwa sisi kutokuwa waaminifu au wakweli katika biashara

Nilikuwa Nina msingi mmoja kuwa

*_si nunui kitu kutoka mkononi mwa mtu / yani ambacho ameshatumia_*

👆kwani nilikuwa naamini sisi waswahili mtu hauzi kitu isipokuwa kikianza kumletea matatizo

1) mtu akiona gari yake ishaanza kuwa mbovu au inakunywa mafuta utasikia anaambiwa bora uiuze

2) mtu laptop yake ikianze kuwa haikai chaji sana utasikia bora niiuze ili ninunue nyengine

4) mtu nyumba yake akiona imekumbwa na vitimbwi vya mashetani Utaskia Acha niuze nitafute Pengine

5) mtu simu yake ikianza kuto kukaa chaji au net haipandi vizuri Utamsikia bora niuze Isije niharibikia mikononi

👆 Sio ubaya kuuza lakini uislamu unakutaka ubainishe udhaifu wa unachouza

💉 Nauza laptop hii lakini haikai chaji sana : inakaa kama dakika 15 tu

Kwaio mtu anahiari anunue au aache

👉 Lakini kutokana na kukosa Tabia njema na mwenendo wa kiislamu leo hii wafanya biashara wa kiislamu tunaongoza kwa udanganyifu na hadaa.

Allah anajua zaidi

•┈┈•┈┈•⊰✿📚✿⊱•┈┈•┈┈•

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 


No comments

Powered by Blogger.