TABIA NJEMA SEHEMU YA 8
🌹 *_رياض الصالحين (SEH:8)_* 🌹
🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
🔻 *_KUWA NA SUBIRA_* 🔻
→ Mengi maovu tunayafanya kwa sababu yaku kosa subira na uvumilivu wakati uislamu unahimiza tuwe na subira katika harakati zetu zote za kimaisha
🎒 Subira imegawika katika sehemu kuu tatu :
① Subira katika utiifu { kumtii Allah }
② Subira katika kujihifadhi na kujilinda na yalioharamu
③ Subira katika lile alilokukadira Allah
▂▂▂▂▂
*_LA KWANZA_* :
→ Mtu anatakiwa awe na subra katika kumtii Allah : kwani katika kutekeleza maamrisho mtu anaweza akaona uzito katika nafsi na mwili wake : Lakini anatakiwa mtu ajitahid na afanye yote ambayo mola wake amemuamrisha
*_LA PILI_*
→ Pia mtu anatakiwa awe na Subira kwa kujiepusha na yale yote ambayo Allah amekataza : kwani nafsi siku zote inaamrisha maovu Kwaio mtu anatakiwa awe mvumilivu na asifuate yale ambayo nafsi inamuamrisha kama vile uongo , kufanya hadaa katika biashara , wizi , kufanya uzinifu , kunywa pombe na mengineyo
*_LA TATU_*
→ Mtu anatakiwa awe na subra kwa lile ambalo Allah amemkadiria : mfano mtu amefukuzwa kazi , amefiliwa na anaempenda , amepatwa na maradhi , mali yake imepotea au kuharibika nk
📜الـــمَــصــــــــــدر
🔍 شرح رياض الصالحين { ١/٧٨ }
•┈•✾•┈•┈••✾
Zimekuja dalili mbali katika katika Quran kuhimiza suala zima lakuwa na Subira kama Allah anavyotubainishia
(❶) " Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Allah, ili mpate kufanikiwa." { 3:200}
(❷) " Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri," { 2:155 }
(❸) " Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu. " { 39:10 }
___
💉 Kwaio Tunapaswa kuwa na Subira kwa kufanya yote yalio mema na kuacha yote yalio maovu , hakika Allah amewaandalia wote wenye Subira malipo makubwa na mazuri
Itaendelea In shaa Allah
_*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*_
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
📚📚
📚
🌹 _*NYONGEZA*_🌹
Siku zote muumini na muislamu wa kweli anatakiwa awe na dhana njema kwa mola wake kwa chochote /lolote ambalo litamtokezea kama mtume ﷺ anavyotubainishia
🔻 *_Ajabu ya jambo la muumini , hakika mambo yake yote ni kheri , wala hakuna Anaepata hilo isipokuwa muumini peke : Akipatwa na furaha hushukuru ikawa ni kheri kwake , na akipatwa na madhara husubiri ikawa { pia } ni kheri kwake_* 🔺 Muslim { 2999 }
💉 Muislamu anapopatwa na msiba , matatizo , majanga , balaa na kila aina ya msiba basi mambo yafutayo anatakiwa ashikamane nayo :
(❶) *_Akae kimya_*
Na huku kukaa kimya au kunyamazia kupo kwa aina mbili :
a} kwa moyo : yani asiwe na hasira na mola wake pia asiwe na dhana mbaya kwa Allah , wala asijetia moyo mwake kuwa Allah hampendi au amemdhulumu nk
b} kwa ulimi : hii mtu anatakiwa baada ya kupatwa na msiba au matatizo asitoe Maneno machafu , au asiombe maangamizo
Mfano Ahhhhh ndo nishafukuzwa kazi bora ningekufa au bora ningeondoka duniani
Au baba ndo usha fariki hakuna wa kunisaidia bora ningetangulia Mim au tungeondoka pamoja nk
❌ Aina hizo zote hazitakiwi pindi mtu anapokumbwa na
au matatizo
(❷) *_Awe na Subira_*
Ukikumbwa na tatizo basi unatakiwa uwe mvumilivu na Allah atakupa mbadala wake ambacho kina kheri zaidi
(❸) *_Uridhie kile ambacho Allah amekupangia_*
(❹) *_Ushukuru_*
→ unatakiwa umshukuru Allah kwa icho ambacho kimetokea au kukupata , hakika mtume wa Allah anapoona kitu ambacho hakimpendezi husema kuwa anamshukuru Allah kwa kila hali
الحمد لله على كل حال
{ sahihi jaami : 4640 }
Kwaio tunatakiwa tumshukuru Allah na Allah atatulipa thawabu na lililobora kuliko hilo ambalo limetukuta.
_____
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments