Header Ads

Header ADS

TABIA NJEMA SEHEMU YA 7

 🌹 *_رياض الصالحين(SEH:7)_*  🌹


🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺

▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂


🔻 *_KUMTEGEMEA ALLAH_* 🔻



→ Katika Tabia na mwenendo mwema na ndivyo uislamu unavyo tufundisha, tumtegemee Allah ukweli wa kumtegemea katika mambo yetu yote 



→ Yoyote anaemtegemea Allah na kumcha kwa kufanya yale alioamrishwa na kuacha yale aliokatazwa basi Allah atamtosheleza na haja zake zote , na ndipo Ibn jubayr aliposema : 



*_Kumtegemea Allah ni katika sifa kuu ya imani_* 



→ zimekuja dalili mbali mbali katika Quran na sunna kuonesha umuhimu wa kumtegemea Allah katika mambo yetu : 


a} iwe wewe ni mwanafunzi unataka kufaulu masomo 


b} iwe wewe ni mfanya biashara unataka biashara zako ziende vizuri 


c} iwe wewe ni mfanya kazi unataka uwepo sehemu nzuri 


d} iwe wewe ni mwanamke unaetaka kuolewa na mume mzuri na mwenye kheri 


👆Yote Hayo unatakiwa umtegemee Allah peke yake : ushirikina , kafara , kuroga , ndumba nk yote hayana nafasi kwa anaemtambua na kumuogopa mola wake


♻ *_✾ ‏قال ابن العثيمين رحمه الله_* :


💉  kumtegemea yeye { Allah } katika mambo yako yote , kwani Allah akiwa haja kufanyia wepesi hakuna Atakae kufanyia wepesi { jambo halitokuwa jepesi } , na sababu ya kukufanyia wepesi *_Ni kumtegemea yeye_* ... na utakapomtegema Allah atakutosheleza kwa kila kitu ...


📜الـــمَــصــــــــــدر

🔍 شرح رياض الصالحين { ١/٢٨٤ } 

_____



‼ *_Enyi !!!!_* wafanya biashara , wauza maduka , wenye dalala dala , wavuvi , wafanya kazi maofisini ushirikina hauna nafasi katika uislamu Bali tunatakiwa tumtegemee Allah haki ya kumtegemea kama kama anavyotuambia yeye mwenyewe : 



۞ *_وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ_* 


_Na humruzuku kwa jiha { namna} asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Allah Yeye humtosha._۞

▂▂▂▂▂



Itaendelea In shaa Allah


_*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*_


https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw


QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A


📚📚


   📚


🌹 _*NYONGEZA*_🌹


Katika Suala la kumuomba au kumtegemea Allah kuna watu wa aina tatu : 



1) wanamuabudu Allah na kutaka msaada kwa Allah 


2) hawataki kumuabudu wala kutaka msaada kwa Allah 


👉 Lakini hawa wanapokumbwa na matatizo hujidai kumuomba Allah kwa lengo la kufanikisha haja zao tu 


3) Wana muabudu Allah lakini kiuhalisia hawataki msaada wa Allah 


👉 waislamu Wengi tumeanguka katika kundi hili 


Utamkuta mtu anaingia msikitini , anafunga ramadhani , ametamka shahada nk lakini 


a} anapotaka kuuza chipsi au kufungua duka lazima kwanza aende kwa mganga 


b} anapotaka kuoa lazima akapige ramli na kuangalia nyota lini na saa ngapi aoe au ambadilishe jina mkewe ili asimtawale 


c} anapotaka kupandishwa cheo kazini lazima amroge wajuu yake kwanza ili nafasi aichukue yeye 


d} anaamini kuwa bila ya uwepo wa Fulani basi Maisha yake yatakuwa duni { atakuwa masikini } 


👆 yoyote ambae yupo katika hili kundi nambari { 3 } basi huyo hayumo katika wale wanaomtegemea Allah katika mambo yao 



Kundi bora ni lile nambari { 1 } ambapo wanamuabudu mola wao na kumtegemea.


_____


QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 


 

No comments

Powered by Blogger.