TABIA NJEMA SEHEMU YA 6
🌹 *_رياض الصالحين (SEH:6)_* 🌹
🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
🔻 *_KUFANYA KAZI_* 🔻
→ Katika Tabia na mwenendo mwema ni mtu kufanya kazi na kula kutokana na chumo halali la mikono yake :
Uislamu umehimiza Suala zima la watu kujishuhulisha na kuacha kujibweteka na kutegemea Kuomba au kumtegemea mtu Fulani , na zimekuja dalili mbali mbali katika Quran na sunna kama ifuatavyo :
🔻 *_USHAHIDI_* 🔻
(❶) " katu hakuna yoyote alikula chakula bora kuliko aliekula kwa kazi ya mkono wake , Hakika mtume wa Allah , daud alikuwa akila kutokana na kazi ya mkono wake " Bukhari { 2072 }
(❷) " Yeye ndiye aliye idhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa." Al mulk { 15 }
*_YAANI_* : tembeleeni katika ardhi iwe nchi au mikoa mbali mbali kwa lengo la kutafuta kipato au biashara au shuhuli nyenginezo za kimaisha lakini huku mkimtegemea Allah katika harakati zenu , kama alivyo tufahamisha mtume ﷺ kuwa kama tutamtegemea Allah ukweli wa kumtegemea basi ataturuzuku kama anavyowaruzuku ndege { ambao wanatoka wakiwa na njaa lakini wanarudi hali wame shiba }
____
Kwaio katika mwenendo mwema ni mtu kufanya kazi na kujishuhulisha na shuhuli mbali mbali ambazo ni halali kwani hata mitume ya Allah ilikuwa inafanya kazi na haingojei kuwaomba watu : kama alivyosema mtume ﷺ
💉 " { nabii } zaka riya alikuwa seremala " Muslim { 2379 }
♻ ✾ قال ابن العثيمين رحمه الله :
→ Na hili linatolea dalili kuwa kazi { kufanya kazi } au kuwa na ujuzi Sio upungufu , kwani mitume عليهم الصلاة والسلام walikuwa wakifanya , na hakuna shaka kuwa hili ndio kheri { bora } kuliko kuwaomba watu ...
📜الـــمَــصــــــــــدر
🔍 شرح رياض الصالحين { ٢/٢٤٨ }
✍ Kwaio Tunapaswa kuachana na Tabia ya utegemezi au Kuomba OMBA bila sababu za kisheria , Bali mtu anatakiwa atumie nguvu zake , akili au maarifa yake na kujishuhulisha na kazi mbali mbali za halali ili ajipatie kipato chake
Itaendelea in shaa Allah
_*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*_
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments