Header Ads

Header ADS

TABIA NJEMA SEHEMU YA 5

 

🌹 *_رياض الصالحين (SEH:5)_*  🌹

🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂

🔻 *_KUWAFANYIA WEMA MARAFIKI WA BABA / MAMA_* 🔻

→ Uislamu unahimiza Sio tu kuwafanyia wema wazazi wawili , Bali pia tuwapende na kuwakirimu rafiki wa wazazi wetu iwe ikiwa wazazi wetu Bado wapo hai au wameshafariki

Na haya ni kutokana na kauli zake mtume ﷺ

🔻 *_USHAHIDI_* 🔻

(❶) " Hakika wema mkubwa ni mtu kuwaunga vipenzi wa baba yake " Muslim { 2552 }

‏♻ ✾ ‏قال ابن العثيمين رحمه الله:

💉 Hakika hadithi hizi vile vile zinaonesha rehma za Allah , kwani wema ni mlango mpana , haihusiki kwa baba na mama tu , Bali hata marafiki wa mama na baba zetu

Ukiwa fanyia wema basi umewakirimu wazazi wako , utapata thawabu ya kuwafanyia wema wazazi

📜الـــمَــصــــــــــدر
🔍 شرح رياض الصالحين { ٢/١٢٧ }
__________

✍ Kwaio tunatakiwa tuwaunge na tuwe nao pamoja wale ambao wazazi wetu walikuwa nao pamoja

Pia tu wafanyie wema marafiki na ndugu wa wazazi wetu.

Pia katika Maisha huwa tunaishi Maisha ya ndoa

Na wakati mwengine hutokezea mmoja kati ya wanandoa akafariki

👉 Basi katika Tabia njema za uislamu unatufunza tuwakirimu na kuwafanyia wema marafiki au mashoga wa wake / waume zetu ambao Tayari wameshafariki

Na hili limethibiti kutoka kwa mtume wa Allah ﷺ kutokana na yale aliosimulia mama Aisha kuwa :

Mtume alipokuwa akichinja mbuzi husema *_wapelekeeni marafiki zake Khadija_*

katika riwaya nyengine zina sema kuwa mtume alikuwa akiwapelekea rafiki zake mama Khadija kiasi kinachowatosha

{ bukhari : 3816 , Muslim : 2435 }

👆Kwaio apo utaona kuwa mtume wa Allah alikuwa akiwakirimu jamaa na marafiki wa mama Khadija
___________

Pia ikitokea ulikuwa na mtoto na ana rafiki zake

Ikatokea amefariki au ameondoka basi pia unaruhusika kuendelea kuwakirimu wale rafiki zake

Kwa mfano kama mwanzo ulikuwa unawaruhusu kuja kula au kukaa ukumbini kucheza

Basi hata kama mwanao hayupo basi unaweza kuwakirimu vile vile ili wasijione wapweke

*RAUDHWATUL ILM*

_*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*_

https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 

No comments

Powered by Blogger.