Header Ads

Header ADS

SWALAH SEHEMU YA 17

 *Assalaam Alaykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh* 




            *ALIVYOKUWA AKISOMA*

              *(صلى الله عليه وآله وسلم)*

💠  *KTK SWALH MBALMBAL* .💠

    

SEHEMU YA KUMI NA SABA



1⃣  *Swalah Ya Adhuhuri*

 Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika Rakaa mbili za mwanzo Suratul-Faatihah na Surah mbili, hurefusha ya kwanza kuliko ya pili.([ *Al-Bukhaairy na Muslim*])

 

Mara nyingine alikuwa akiirefusha urefu ambao ilikuwa inaweza kufika kuqimiwa kwa Swalah ya Adhuhuri, na aliweza mtu kwenda Al-Baqiy' kukidhi haja yake, [kisha aende nyumbani kwake], kutawadha, kisha aje hali ya kuwa Mjumbe wa ALLAAH (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa bado yuko katika Rakaa ya mwanzo, kwa namna alivyokuwa akiirefusha ([ *Muslim na Al-Bukhaariy katika Juz-u Al-Qiraat (Makala ya Tilaawah)*]).

 

(Pia) walikuwa wakidhania kwamba alikuwa akifanya hivyo ili watu waweze kuidiriki Rakaa ya mwanzo.([ *Abu Daawuud ikiwa na isnaad Swahiyh na Ibn Khuzaymah (1/165/1).*])

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika kila Rakaa ya hizo Rakaa mbili, kadiri ya Aayah thelathini, kiasi cha kusoma As-Sajdah [32-30] na ikiwemo al-Faatihah. (na kufuatia As-Sajdah [32-30])

 

Mara nyingine alikuwa akisoma:-


*((وَالسَّمَاء وَالطَّارِقِ))*

 

*((Naapa kwa mbingu na kinachokuja usiku!))* [At-Twaariq: 86-17],  na

 

 

*((وَالسَّمَاء ذَاتِ الْبُرُوجِ))*

 

*((Naapa kwa mbingu yenye Buruji!))* [Al-Buruuj: 85-22],  na

 

*((وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَى))*

 

*((Naapa kwa usiku unapo funika!))* [Al-Layl: 92-21], na mfano wa Surah zilizofanana na hizi.([ *Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na Ibn Khuzaymah (1/67/2)* ])

 

Na huenda akasoma


 *((إِذَا السَّمَاء انشَقَّتْ))*

 

*((Itapochanika mbingu)) [Al-Inshiqaaq: 84-25], na mfano wake*. [(Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1/67/2)])

 

Walikuwa wakiweza kuelewa kwamba alikuwa anasoma katika Adhuhuri na Alasiri kutokana na mtikisiko wa ndevu zake.([ *Al-Bukhaariy na Abu Daawuud* )] 

 

 

In Shaa ALLAAH tutaendelea tena  biidhiniLLAAHI. 


https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk



QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.