Header Ads

Header ADS

SWALAH SEHEMU YA 18

 *A'ssalam alaykum Wa Rahamatullaah Wa Barakatuh*



KISOMO CHAKE* 

                 *(صلى الله عليه وآله وسلم)*

     *KATIKA SWALAH ZA ALASIRI,*

💠   *MAGHARIB NA 'ISHAA*   💠 

SEHEMU YA KUMI NA NANE

============♦===========


 

2⃣   *SWALAH YA ALASIRI*

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika Rakaa mbili za mwanzo al-Faatihah na Surah mbili, hurefusha Rakaa ya kwanza kuliko ya pili na walikuwa wakidhani kuwa alikuwa akifanya hivyo ili watu waweze kuidiriki Rakaa ya mwanzo.([ *Ahmad na Muslim* ])

 

Alikuwa akisoma kadiri ya Aayah kumi na tano katika kila Rakaa mbili za mwanzo, kiasi cha nusu ya kisomo alichokuwa akisoma katika Rakaa mbili za mwanzo za Swalah ya Adhuhuri, na alikuwa akizifupisha Rakaa mbili za mwisho kiasi cha nusu ya urefu wa Rakaa mbili za mwanzo.([ *Ahmad na Muslim*])

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma al-Faatihah katika Rakaa mbili za mwisho. Alikuwa akiwasikilizisha Aayaah (au zaidi) mara nyingine, na alikuwa akisoma Surah tulizozitaja hapo nyuma katika Swalah ya Adhuhuri.

 

 

 

3⃣  *SWALAH YA MAGHRIB*

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika Swalah hii – baadhi ya nyakati -Surah fupi za Mufasswal, kiasi cha *“wao wanapomaliza kuswali naye, huondoka mmoja wao, na hakika mtu (angeweza kuutupa na) kuona sehemu iliyoangukia mshale wake*.”. 

 

Na (Mara moja), alipokuwa safarini alisoma:-

 

*((وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ))*

 

*((Naapa kwa tini na zaytuni!)) [At-Tiyn 95:8) katika Rakaa ya pili*.([ Atw-Twayaalisy na Ahmad katika isnaad Swahiyh )] 

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) mara nyingine akisoma Surah ndefu za Mufasswal na za wasitani, hivyo alikuwa akisoma:

 

*الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ*

 

*((Waliokufuru na wakazuilia njia ya ALLAAH ))*. [ ( Muhammad 47: 1].

 

Mara nyingine akisoma Suratu-Twuur [52: 49]

 

Na mara nyingine akisoma Suratul-Mursalaat [77: 50] ambayo aliisoma katika Swalah (yake) ya mwisho aliyoiswali (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma moja kati ya Surah mbili ndefu (atw-Twuwlayayn)([12]);  [Al-A'araaf 7: 206] (katika Rakaa mbili).  Na mara nyingine akisoma Al-anfaal [8: 75] katika Rakaa mbili.




https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 *KISOMO KATIKA SUNNAH* 

            *(BAADA YA SWALAH)* 

                              *YA*

                     *MAGHARIBI*

=============♦=============.  

Ama katika Sunnah ya baada (al-ba’diyyah) ya Maghrib, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma:-

 

*((قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ))*


*((Sema: Enyi makafiri!))*. [Al-Kaafiruun 109: 6],  na

 

 

*((قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ))*


*((Sema: Yeye Allaah ni wa Pekee))*. [Al-Ikhlaasw 112: 4].

 

  

4  *SWALAH YA 'ISHAA*

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surah za kati na kati za Mufasswal katika Rakaa mbili za mwanzo, hivyo alikuwa mara nyingine akisoma:-

 

 

*((وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا))*


*((Naapa kwa jua na mwangaza wake!))*  [Ash-Shams 91: 15] na Surah nyingine zilizofanana na hiyo.

 

Na mara nyingine alikuwa akisoma:

 

*((إِذَا السَّمَاء انشَقَّتْ))*

 

*((Itapochanika mbingu)) [Al-Inshiqaaq 84: 25)*, na alikuwa akileta Sajdah humo.

 

Pia mara moja alipokuwa safarini alisoma:

 

*((وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ))*


*((Naapa kwa tini na zaytuni!))* [At-Tiyn 95:8) (katika Rakaa ya mwanzo).

 

 

Alikataza (صلى الله عليه وآله وسلم) kurefusha kisomo katika 'Ishaa, katazo hili lilikuja wakati Mu'aadh bin Jabal alipowaswalisha watu wake Swalah ya 'Ishaa akaifanya ndefu, akajiondoa mtu mmoja katika Answaar na kuswali pekee. Mu'aadh akaelezwa habari ya mtu huyo akasema: *"Hakika yeye ni mnafiki"*. Mtu yule ilipomfikilia taarifa, alikwenda kwa Mjumbe wa ALLAAH (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumweleza vile alivyosema Mu'aadh. Basi hapo Mtume  (صلى الله عليه وآله وسلم)akamwambia Mu'aadh: ((Je, unataka kuwa mfitini ewe Mu'aadh? Utaposwalisha watu basi soma:

 

 

*((وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا))*


*((Naapa kwa jua na mwangaza wake!))*  [Ash-Shams 91: 15], na

 

 

*سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى*

 

*((Litakase Jina la Mola wako Aliye juu kabisa))* [Al-A'laa 87: 19], na

 

 

*((وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَى))*

 

*((Naapa kwa usiku unapofunika!)) [Al-Layl 92: 21] [Bila ya shaka huswali nyuma yako watu wazima, wagonjwa na wenye haja zao*].

 

 In Shaa ALLAAH tutaendelea tena



https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 


No comments

Powered by Blogger.