SWALAH SEHEMU YA 19
*Assalaam A'laykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*
*KISOMO CHAKE*
*(صلى الله عليه وآله وسلم)*
*KATIKA SWALAH YA WITR*
💠 *SIFA YA SWALAH YA MTUME* 💠
SEHEMU YA KUMI NA TISA
============♦===========.
*SWALAH YA WITR*
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akisoma katika Rakaa ya mwanzo:
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى
*((Litakase Jina la Mola wako Aliye juu kabisa))* [Al-A'laa 87: 19],
na katika Rakaa ya pili:
*قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ*
*((Sema: Enyi makafiri))* [Al-Kaafiruun 109: 6],
na katika Rakaa ya tatu.
*((قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ))*
*((Sema: Yeye ALLAAH ni wa Pekee))* [Al-Ikhlaasw 112: 4].
Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiongeza katika Rakaa ya mwisho kwa kusoma:
*قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ*
*((Sema: Najikinga kwa Mola wa mapambazuko))* [Al-Falaq 113: 5],
na
*قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ*
*((Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wana Aadam))* [An-Naas 114: 6] ([2]).
Na mara nyingine alisoma katika Rakaa ya tatu Aayah mia kutoka katika Suratun-Nisaa [4: 176]
Ama zile Rakaa mbili baada ya Witr, alikuwa kaisoma ndani yake:
*إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا*
*((Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake)*) [Az-Zilzalah 99: 8], na
*قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ*
*((Sema: Enyi makafiri))* [Al-Kaafiruun 109: 6]
*KISOMO CHAKE*
*(صلى الله عليه وآله وسلم)*
*KATIKA SWALAH YA IJUMAA*
============♦=============
*SWALAH YA IJUMAA*
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akisoma mara nyingine katika Rakaa ya mwanzo Suratul-Jumu'aa [62: 11]:
*يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿١﴾*
*((Vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi vinamtukuza ALLAAH , Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikmah)),*
na katika Rakaa ya pili:
*إِذَا جَاءكَ الْمُنَافِقُونَ*
*((Wanapokujia wanaafiki))* [63: 11]([ Muslim na Abu Daawuud ]),
na mara nyingine - badala yake) - alikuwa akisoma:
*هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ*
*((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?))* [88: 26],
na mara nyingine akisoma:
*سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى*
*((Litakase Jina la Mola wako Aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87: 19]*,
katika Rakaa ya mwanzo na:
*هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ*
*((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?))* [88: 26],
katika Rakaa ya pili([ Muslim na Abu Daawuud ]).
In shaa ALLAAH tutaendelea tena biidhiniLLAAHI
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments