SWALAH SEHEMU YA 20
*Assalaam Alaykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*
Na'am tunaendelea na darasa letu
*KISOMO CHAKE*
*(صلى الله عليه وآله وسلم)*
*KATIKA SWALAH ZA 'IYD MBILI*
💠 *SIFA YA SWALAH YA MTUME* 💠
*SEHEMU YA ISHIRINI*
=============♦============
*SWALAH ZA 'IYD MBILI*
"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akisoma (mara nyingine) katika Rakaa ya kwanza
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى
*((Litakase jina la Mola wako Aliye juu kabisa))* [Al-A'laa 87: 19],
na katika Rakaa ya pili:
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ
*((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?))* [88: 26] [1].
Na mara nyingine "alikuwa akisoma katika hizo Rakaa mbili:-
ق وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ
*((Qaaf, Naapa kwa Qur-aan Tukufu))*[Qaaf 50: 45], na
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ
*((Saa imekaribia na mwezi umepasuka))* [Al-Qamar 54: 55]
*KISOMO CHAKE*
*(صلى الله عليه وآله وسلم)*
*KATIKA SWALAH*
*YA JANAAZAH*
============♦============
*SWALAH YA JANAAZAH*
"Sunnah ni kusoma Suratul Faatihah [na sura nyingineyo] . Pia *"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikaa kimya kwa muda baada ya Takbiyr ya kwanza"* [( An-Nasaaiy na At-Twahaawiy)]
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
*KUSOMA KISOMO VILIVYO*
*NA*
*KUITENGENEZA SAUTI*
*UNAPOSOMA*
============♦============
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma - kama Alivyoamrishwa na ALLAAH - Qur-aan vilivyo – kama inavyotakiwa kusomwa, mtu anatakiwa achunge hukumu za kuisoma-, bila ya kwenda mbio wala kuharakiza, bali kisomo cha "Uchambuzi/ufafanuzi chenye kupelekea kubaini herufi baada ya herufi" (sana) hadi "alikuwa akisoma Surah mpaka inakuwa ndefu mno kulinganisha na Surah iliyo refu na hiyo anayoisoma (kwa kadiri inavyowezekana).
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: *((Itasemwa kwa mwenye kusoma Qur-aan (siku ya Qiyaamah): Soma na upande; soma (pole pole kwa mahadhi) kama ulivyokuwa ukisoma duniani; makaazi yako kwenye Aayah ya mwisho usomayo))*[ Muslim na Maalik ]
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) "akirefusha kisomo chake (kwenye herufi za kurefushwa), alikuwa akirefusha Bismi Llaahi, na akirefusha Ar-Rahmaan na akirefusha Ar-Rahiym" na katika "nadhiyd" [Qaaf 50: 10][8] na mfano wa (kama) hizo.
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisimama mwisho wa kila Aayah kama ilivyoelezwa kabla.
Mara nyingine "alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma kwa sauti ya kuvutia ya kutetema kama alivyofanya siku ya kufunguliwa kwa Makkah hali ya kuwa yuko juu ya ngamia wake, anasoma Suratul-Fat-h [48: 29] [kwa sauti nyororo] na 'Abdullaah bin Mughaffal amesimulia hii sauti ya kuvutia : aaa" [ Bukhariy na Muslim ]
Alikuwa akiamrisha kuipamba sauti katika kusoma Qur-aan, alikuwa akisema: *((Ipambeni Qur-aan kwa sauti zenu (kwani sauti nzuri huzidisha kuipamba Qur-aan))*[ Al Bukhariy ]
Na alikuwa akisema: *((Hakika mwenye sauti bora miongoni mwa watu katika kusoma Qur-aan ni yule ambaye mnapomsikia akiisoma, mtamdhania ni mwenye kumkhofu ALLAAH ))*
Alikuwa pia akiamrisha kusoma Qur-aan kwa sauti ya kupendeza, alikuwa akisema: *((Jifunzeni kitabu cha ALLAAH , dumisheni kuisoma, ithibitisheni (kuhifadhi), na isomeni kwa (sauti ya) kughani, kwani Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, inakimbia haraka kuliko ngamia anavyochopoka katika kamba))* [( Ad-Daarimiy na Ahmad kwa isnaad Swahiyh.)]
Alikuwa pia akisema: *((Sio miongoni mwetu mwenye kuisoma Qur-aan bila ya kughani [kupendezesha sauti]))* [( Abu Daawuud na al-Haakim)]
Na akisema:
*((ALLAAH Hakuwahi kusikiliza kitu chochote zaidi ya jinsi ya kusikiliza* [katika riwaaya nyingine: *((Kama Anavyomsikiliza))] Mtume (kwa shauku) ((kwa sauti ya kupendeza))]*, na [katika riwaaya nyingine: *anavyosoma Qur-aan kwa sauti nzuri[16] ((ananyanyua sauti kwako))* [( Al-Bukhaariy, Muslim, At-Twahaawiy na Ibn Mandah katika Tawhiyd (81/1)) ]
Alimuambia Abu Muusa Al-Ash'ariyy (رضي الله عنه) *((Lau ungeliniona nilipokuwa nasikiliza kisomo chako usiku wa jana, kwa Hakika umepewa mzumari katika mizumari ya aila ya Daawuud!))* Hivyo Abu Muusa akasema: *"Lau ningelijua kuwa uko, ningelizidi kuitengeneza na kuipendesha sauti yangu kwa ajili yako*" [( 'Abdur-Razzaaq katika Al-Amaaliy (2/44/1), Al-Bukhaariy, Muslim, Ibn Naswr na Haakim.]
In shaa ALLAAH tutaendelea tena biidhiniLLAAHI
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
*Ungana nasi kupitia channel yetu mpya ya Telegram ili kupata darsa zoot za SWALAH*
⬇⬇
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments