Header Ads

Header ADS

TUIJUE MASJID AL SQSWA

 Tuijue Masjid Al Aqswa


Masjid Al Aqswa au kwa jina lengine Baitul Maqdis ni msikiti watatu bora duniani na wapili kujengwa baada ya msikiti wa Makkah na pia ni Qibla cha kwanza cha Uislamu.


Msikiti huu uko katika Mji wa Al-Quds (Jerusalem) katika ardhi ya shaam ambayo kwa sasa ni nchi inayoitwa #Palestine na wala haiko Israel kwani duniani hakuna nchi inayoitwa Israel, bali ni mayahudi na mabwana wao wamagharibi baada ya kuvamiya palestina ndio wakaanza kuita israel na kusema katika mitandao kuwa masjid Al Aqswa uko Israel.


Kutoka kwa Abu Darda (RA) Mtume (ﷺ)  asema: " Swala moja katika msikiti wa Makkah ni bora kushinda swala 100,000 za sehemu yengine, na swala moja ya msikiti wangu wa madina ni sawa na swala 1000, na swala moja masjidul Aqsa ni sawa na swala 500 sehemu yengine. (Bayhaqi)


Abu dharr (RA) asimulia alipomuuliza mtume (ﷺ), "Ewe mtume wa Allah, misikiti gani ni wa kwanza kujengwa duniani?," Mtume (ﷺ) akamjibu, "Masjid Haram" akauliza tena "Kisha ni gani?" Akajibiwa ni "Masjid Aqswa" Akauliza tena, tafauti yao ya kujengwa ni miaka mingapi?" Akajibiwa "Ni miaka Arubaini."

(Bukhari na Muslim)


Maulama walitafautiana kuhusu nani aliyejenga wa kwanza, kama kina Ibn Hajar wakasema ni Nabii Adam (AS) na wengine wakasema ni Mtume Yaakub (AS) kisha ikafwatiliwa kujengwa na Nabii Suleiman (AS).


Lakini pale wanahistoria watareh walipo anza kuchukuwa historia ya msikiti huu vizuri wanasema msikiti huu ulikuwepo toka zamani, Mtume (ﷺ) alisafirishwa usiku wa isra wal miiraj hadi hapo na kuswalisha mitume wote 124,000/-. 


Katika Khilafah ya Umar (Ra) aliufungua mji wa Al-Quds na kujenga vizuri sehemu ya kuswali, na sehemu hiyo kupanuliwa majengo kila zama za makhalifa wengine na baadhi ya miaka majengo hayo ikiharibiwa na mitetemeko ya ardhi au kuharibiwa na maadui na kisha kuinuliwa mijengo mipya. 


Mwaka 1099 miladiya Makruseda waliuchukuwa mji wa Alquds (Jerusalem) na kuchafua masjid Aqswa kwa kufanya ni mahekalu yao ya uchafu, kisha mwaka 1187 miladiya Salahudeen Al-Ayubi (RA) aliukomboa mji wa Jerusalem baada ya vita vikali na makruseda hatimaye aliurudisha mji wa jerusalem kwa waislamu.


Katika hiyo picha ya Masjid Al Aqswa inaonyesha nambari katika kila jengo ambayo tutaeleza kwa uzuri kila jengo hapo na umuhimu wake.


1. Masjid Al Aqswa (Aqsa Precinct/Sanctuary).

Masjid Aqswa ni ardhi yote hiyo iliyozungukwa na hilo boma lililochorwa kwa rangi ya Machungwa, kawaida tumezowea kusikia masjid aqsa na kuona ni jengo flani, lakini laa masjid aqsa ni hilo boma lote ni tukufu kwa mujibu wa Quran. Ambalo ndani yake kuna majengo takriban 44 pamoja na Masjid Qibly (Masallah Aqsa) na Qubbat al-Sakhra (Dome of Rock).


Mtu anaweza kuuliza mbona kiwanja pekee kiitwe masjid Al aqswa? 


Jibu hata Masjid Haram wakati wa mtume SAW kulikua na Kaaba tu kisha baadae ndio kukajengwa msikiti uliozunguka Kaaba na Eneo zima hilo lina tambulika kama masjid Haram.


Kadhalika Qubbatul sakhara iliojengwa na Abdul malik bin marwan pamoja na Masjid Al qibliy zote ziko ndani ya Masjid Al aqswa


Wenyeji wa huko huita sahemu hii Haaram Al-Shareef, kwa ule utukufu wake. Inaaminika masjid Al Aqswa kuwa na ukubwa wa mraba mita 144,000 (SQ meter) na kokote utakaposwali katika hilo boma utapata fadhila ya swala moja ya hapo kuwa sawa na swala 500 za Misikiti mengine isipokuwa Masjid Haraam na masjid Nabawi.


Chanzo: 

https://www.islamiclandmarks.com/palestine-masjid-al-aqsa/masjid-al-aqsa


2. Qubbat Al-Sakhara (Dome of the Rock).

Hili ni jengo lenye mnara wa rangi ya dhahabu katika hiyo picha, hili ndio jengo linalowachanganya sana waislamu. Na kila mmoja kuwa na fikra tafauti kuhusu hili jengo. Wengine husema ni kanisa, hekalu la mayahudi, Masjid Al Aqswa au mnara wake wote ni wa dhahabu.

Lakini yote si kweli ila ukweli ni kuwa, hili ni jengo ambalo lipo ndani ya eneo la masjidul Aqswa. Inaaminika kuwa zamani sehemu liliopo jengo hili kulikuwa na mlima wenye jiwe juu yake, jiwe ambalo lina aminika ndilo aliposimama Mtume SAW na Jibril AS kupaa juu mbinguni kuelekea safari ya miiraj.


Kwa sababu ya utukufu wa mlima huu na jiwe lake kulijengwa juu yake Jengo hili (Qubat Al-Sakhara/Dome of the Rock) na Khalifa AbdulMalik ibn Marwa (RA) mwaka 691-692 miladiya. Alijenga jengo hili kwa urembo mzuri sana kwa sababu waislamu wakati huo walikuwa wameendelea katika fani ya ujenzi na mapambo, akaja mtoto wake Al walid bin abdulmalik mwaka 705 miladiya naye akaiboresha zaidi na kila zama za makhalifa zikipita jengo hili likiboreshwa.


Pia ndani ya jengo hili waislamu huswali kwa kueleka qibla cha makkah na sana sehemu hii hutumiwa na wanawake kuswali. Kwa hivyo hili si kanisa wala hekalu (temple mount) kama vile mayahudi na baadhi ya waislamu hudai katika mitandao.


Chanzo: https://www.islamiclandmarks.com/palestine-masjid-al-aqsa/the-dome-of-the-rock


3. Masjid Qibly (Masallah Al-Aqsa).

Hili ni jengo lenye mnara mweusi au kijivu juu yake. Jengo hili baadhi ya waislamu bila ya kujua wao husema ndio Masjid Aqswa. Lakini hili pia ni jengo liliopo ndani ya masjid aqswa upande wa Mbele. 


Jengo hili lilianzishwa na Saydna Omar (RA) alipoifatih AlQuds (Jerusalem) kutoka kwa warumi mwaka 638 Miladiya aliamrisha kujengwa sehemu itakayokuwa na kivuli watu wapate kuswali. Kukajengwa jengo la mbao sehemu hiyo na kuja baadae kujengwa jengo hilo kwa matofali na kulifanya jengo hilo kuwa madhubuti wakati wa Khalifa Abdul Malik mtoto wa walid (RA) mwaka 705-715 miladiya.


Jengo hili hutumiwa kama sehemu ya kuswalia wanaume katika masjid Al aqswa.

Hivyo basi Masjid Al Aqswa sio jengo bali ni kiwanja chote mukionacho katika hiyo picha na majengo yote humo ndani yake yana daraja na utukufu sawa hadi miti na michanga yake. Kwa kauli yake Allah SWT Aliposema:

 "SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Harram mpaka Msikiti Al Aqswa, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka," (Surah Al- Isra':1)


Chanzo:

https://www.islamiclandmarks.com/palestine-masjid-al-aqsa/masjid-al-qibly


4. Musallah Marwani

Hili ni jengo liliyopo upande wa mashariki pamoja eneo la chini ya masjid Qibly linaaminika kutengezwa wakati wa Nabii Suleiman (As) na kuja kurekebishwa na Khalifa Marwan (RA) na kupewa jina hilo kwa ajili yake.


Sehemu hii ya chini pia inatumiwa kuswalia kwa sababu ya ukubwa wake unaoweza kubeba takriban waislamu 10,000.


Chanzo: https://www.islamiclandmarks.com/palestine-masjid-al-aqsa/marwan-e-masjid


5. Masjid Al Buraq

Jengo hili dogo liko upande wa Kusini magahrib, ambalo hutumika kuswalia. Jengo hili liko Sehemu inayoaminika Mtume (ﷺ) kumfunga Buraq (Mnyama aliyempanda wakati wa Israa wal Miiraj) na pia kuna mlango aliyoitumia kuingilia Masjid Al Aqsa kuswalisha Mitume wengine.


Chanzo: https://www.islamiclandmarks.com/palestine-masjid-al-aqsa/buraq-masjid


Kwa hivyo twafaa kuelewa kama waislamu matukufu yetu na vizuri tufunge safari za kuzuru sehemu hiyo kama vile alivyotunasihi Mtume (ﷺ). 

Katika hadith iliyopokelewa na Abu Hureira (RA), kuwa Mtume (ﷺ) alisema, "Safari nzuri za kuzuru ni katika Masjid Harram, Misikiti wangu huu (Masjid Nabawi) na Masjid Al Aqsa.

(Bukhari na Muslim)


Leo hii waislamu tumechanganywa akili na wamagharibi kuhusu matukufu yetu huku wakituandikia na kutuonyesha vitu vya urongo kuhusu msikiti huu mtukufu katika mitandao na vyombo vyao vya habari.


Pia ni masikitiko makubwa leo hii msikiti huu mtukufu uko chini ya himaya ya mayahudi Mazayuni wazuia na kuruhusu waislamu kuswali vile wanavyotaka, na kuwaruhusu mayahudi wenzao kufanya ziara humo na kuunajisi wanavyotaka, huu ni udhalilifu mkubwa leo hii kwa ummah wa kiislamu. 


Hakika Qadhia hii ya Palestina na Masjid Al Aqsa siyo ya wapalestina pekee  ali ni Qadhia ya uislamu inatuhusu waislamu waulimwengu mzima, lakini leo kwa sababu ya mipaka tuliyochorewa na makafiri na kuwekwa viongozi makhain katika nchi za waislamu ndio qadhia hii haitupelekei kujali kinachoendelea huko wala kujua matukufu yetu yanayo chafuliwa.


Namuomba Allah SWT Atuunganishe mioyo yetu na Atujaalie kusimamisha tena Dola ya kiislamu ya Khilafah alaa minahji nubuwa ili kujakuikomboa tena Masjid Aqswa na kuiregesha mikononi mwa waislamu, kwani Khilafah pekee ndio yenye uwezo wa kuikomboa wala siyo viongozi wanafiq na makhain.


 ALLAHUMA AMEEN!


Imeandikwa na SAAD ABUBAKAR


WASAMBAZAJI

QURAN NA SUNNAH BLOGGER 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBLEA BLOGGER YETU KWA KUSOMA DARASA ZETU ZAIDI

 http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

No comments

Powered by Blogger.