SWALA YA EID SEHEMU YA 6
6⃣ *DUA YA ISTIFTAH*
➡ Kawaida katika swala za faradhi , baada yakuleta takbira yakuhirimia swala ndipo tu naanza kusoma dua ya istiftah Kabla yakuanza kusoma suratul fat-ha
➡ Ama katika swala ya eid , kuna Ikhtilaf za wanavyuoni Lakini wanavyuoni Wengi wameenda kuwa unatakiwa ulete dua hio baada yakumaliza takbira ile ya mwanzo (yakuhirimia swala)
✍ Ingawa wapo baadhi Walosema kuwa unaweza ukaileta baada ya takbira ya mwisho katika zile takbira za eid
*REJEA*
مجموع فتاوى ، ابن العثيمين
المجلد السادس عشر
7⃣ *KUMKUTA IMAMU KATI KATI*
✍ Sio watu wote ambao wanaanza na Imamu tangia mwanzo
✍ Wengine Imma kwa makusudi au kwa bahati mbaya wanachelewa kufika viwanjani na wakifika tayari swala imeshaanza
👊🏿 Utakapomkuta Imamu. yupo katika rukuu : utaleta Takbira yakuhirimia swala tu kisha utamfata Imamu katika rukuu au katika sijda au itidali
👊🏻 Utakapokuja na ukamkuta Imamu yupo katika kisimamo : lakini kisha leta baadhi ya takbira
☝ Unachotakiwa wewe Lete takbira yakuhirimia swala kwanza , kisha mfate Imamu katika takbira zilizobaki , ama zile zilizokupita zitakuwa zimeshadondoka na umesameheka na hutozilipa
*REJEA*
مجموع فتاوى ، ابن العثيمين
المجلد السادس عشر (٢٤٥)
8⃣ *KUKOSA RAKAA KATIKA EID*
✍ Kuna wakati unafika katika viwanja vyakuswalia na unamkuta Imamu kishaanza kuswalisha
✍ Na kwa bahati mbaya unamkuta rakaa moja tayari kishaimaliza wewe unawahi moja tu , je utaikamilisha vipi ?
✍ Utaikamilisha kwa mtindo kama ule alioswalisha Imamu bimaana rakaa utayoikamilisha kama Ni yapili basi na wewe utaleta Takbira tano kama ambavyo Imamu aliswalisha
✍ Lakini pia kama umehifadhi Quran utasoma pia sura zile zile za sunna kuzisoma katika swala za eid : ama kama huzijui basi utasoma kile Allah alichokukadiria
*REJEA*
مجموع فتاوى ، ابن العثيمين
المجلد السادس عشر ( *٢٦٨* )
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments