Header Ads

Header ADS

SWALA YA EID SEHEMU YA 9

 

9⃣ *SURA ZA KUSOMA KATIKA SWALA YA EID*

✍ Watu wakisoma sura zozote zile : swala yao Ni sahihi na Allah atawalipa ujira

✍ Lakini kuna sura Ni sunna na Inapendezeshwa kuzisoma katika swala ya eid

1⃣

  ١) سبح اسم ربك الأعلى

✍ hio itasomwa katika rakaa ya kwanza

٢) هل أتئك حديث الغشية

✍ hio utasoma katika rakaa ya pili

🍃 Baada ya Imamu kumaliza kusoma suratul fat-ha atasoma sura hizo. na Hayo Ni kutokana na hadithi ya Nuuman Bin bashir aliesema kuwa

Alikuwa Mtume salallahu alayhi wasallam. Katika swala za eid na ijumaa alikuwa akisoma sura hizo

2⃣

☝kama Imamu hajasoma sura zile basi zipo sura nyengine Ni sunna kuzisoma baada kumaliza kusoma suratul fat-ha

١) ق

✍ Rakaa yakwanza atasoma suratul Qaaf

٢) القمر

✍ Rakaa ya pili baada kumaliza kusoma suratul fat-ha ataisoma sura hio

*REJEA*

١) مسلم : (٨٩١) ، (٨٧٨)

٢) مجموع فتاوى ، ابن العثيمين

المجلد السادس عشر ( ٢٤٥)

1⃣0⃣ *KHUTBA YA EID*

✍ Swala ya eid nayo imewekewa sheria kwa kuletwa khutba kwa lengo la kuwa waidh watu na kuwapa NASAHA mbali mbali

✍ Lakini Ni tofauti na Ijumaa : siku ya eid watu wataanza kuswali kwanza kisha ndio patasomwa Khutba na huu ndio mwenendo sahihi wa Mtume (salallahu alayhi wasallam )

✍ Amesema Imam At-tormidhiy :

*kinachofanyiwa kazi na watu wenye elimu katika maswahaba wa mtume na wengineo Ni kuswali swala ya eid Kabla ya khutba*

☝na JUU ya hilo zimekuja dalili mbali mbali zinazoonesha kuwa Huo ndio mwenendo wa wema waliotangulia

👊 Kutoka kwa Ibn Umar amesema

*_Alikuwa mtume salallahu alayhi wasallam, na abubakar, na Umar wakiswali eid Kabla ya khutba_*

✍  Kutokana na hilo 👇

👊 Inapendezeshwa watu kubakia katika safu zao  kusikiliza khutba, na bahati mbaya watu Wengi wakimaliza kuswali wanaondoka bila kusikiliza mawaidha na NASAHA za eid ,

☝Hakuna shaka kuwa wanajikimbiza Wenyewe katika kheri , na wanajiepusha na fadhila nyingi

*kwa ufupi* : lengo la kuswali pia nikupata mawaidha na NASAHA za eid , hivyo watu tujitahid kukaa na kusikiliza khutba na wala tusiwe na haraka za kuondoka

*REJEA*

البخاري : (٩٦٣)

مسلم : (٨٨٨)

توضيح الاحكام ( ٢/٢٤٣)

*NYONGEZA*

✍ hapo katika khutba ya eid kuna vitu vingi Tunapaswa tuvijue , baadhi ya hivyo Ni :

1) *je khutba hio Ni wajibu* ?

✍ Hapana , licha ya Ikhtilaf zilizopo lakini kauli yenye nguvu Ni _Sunna_

2) *Zinatakiwa ziwe khutba ngapi* ?

✍ Wapo wanaosema khutba za eid Ni mbili na wapo wanaosema Ni moja , lakini kauli yenye nguvu Ni khutba ya eid Ni moja tu

3) *Inaruhusika kuongea wakati khatib unazungumza* ?

✍ Jibu linatokana na khitilaf zilizopo : kwa wanaoona khutba Ni wajibu basi wanaona kuwa Ni wajibu kukaa kimya na kusikiliza

Kwa wanakona Ni sunna wanaona mtu hapati dhambi akiongea

*lakini* : si katika adabu kuwa khatib anazungumza na wewe unaongea

Kwa ufupi watu wawe kimya wamsikilize khatib Kwani mtu akiongea atajishuhulisha na atawashuhulisha na wengine

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 

No comments

Powered by Blogger.