SWALA YA EID SEHEMU YA1
1⃣ *WAPI INASWALIWA SWALA YA EID*
✍ Sunna nikuswali swala ya eid katika viwanja , yani nje ya msikiti , sehemu ambayo iliokuwa pana na itawakusanyisha waislamu wote ili kudhihirisha utukufu wa Uislamu
✍ Wanaruhusika waislamu wote wanawake , wanaume, watoto, waliokuwa katika siku zao , na waliokuwa tohara wote kuhudhuria katika viwanja panaposwaliwa swala ya eid
✍ Ama waliokuwa katika ada zao wao watu wakiswali hawatoswali Bali wanaruhusika kusikiliza khutba , Kuomba dua na kuleta adhkari mbali mbali
✍ Kuhusiana na kuswali swala ya eid katika viwanja , hii ndio ilikuwa ada ya mtume (salallahu alayhi wasallam na jambo hilo limethibiti katika hadithi nyingi. Miongoni mwa hizo Ni :
🍃 Kutoka kwa Abi said (radhi za Allah ziwe JUU yake ) amesema :
*Alikuwa mtume (salallahu alayhi wasallam) akitoka siku ya fitri na adh-ha katika musalla ....."*
☝ Kutokana na hadithi hio tunajifunza kuwa Ni sunna kuswali eid viwanjani labda kukiwa na dharura basi tutaswali misikitini
*MARRJEO*
الفقه الميسر ( ١.٨)
فقه السنة (١/٣٧٨)
2⃣ *IDADI YA TAKBIRA KATIKA SWALA*
✍ Katika swala ya eid kwa mujibu wa hadithi ya mtume salallahu alayhi wasallam Imamu ataleta Takbira saba katika rakaa ya kwanza
✍ Na katika rakaa ya pili ataleta takbira tano ,
Inaendelea
*+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments