SWALAH SEHEMU YA 22
*Assalaam A'laykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*
Tunaendelea na darasa letu Swalah Leo tupo katika rukuu
*KURUKUU*
*SIFA NA ULAZIMA*
*WA*
*KUTULIA KATIKA RUKUU*
SEHEMU YA 22
=============♦=============.
*KURUKUU*
Baada ya kumaliza kisomo chake (صلى الله عليه وآله وسلم), alikuwa akinyamaza kinyamazo kidogo, kisha huinua mikono yake kwa namna zilizotangulia kuelezwa katika 'Takbiyr Ya Kufungulia, akaleta Takbiyr na akarukuu.
Na pia alimuamrisha mambo mawili hayo aliyeswali vibaya kwa kumwambia: *((Hakika Swalah ya mmoja wenu haitotimia mpaka akamilishe wudhuu vizuri kama Allaah Alivyoamrisha… kisha alete Takbiyr, amsifu na kumtukuza Yeye, na asome kiasi kinachosahilika tu kwake katika Qur-aan miongoni mwa Aliyofunzwa na ALLAAH (kwa kiasi cha wepesi) na uwezo wake, kisha alete Takbiyr na arukuu [na aweke mikono yake miwili juu ya magoti yake mawili] mpaka viungo vyake vitulie na vipumzike…))* [( Abu Daawuud na An-Nasaaiy)]
*SIFA YA RUKUU*
============♦============
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akiweka viganja vyake juu ya magoti yake
na alikuwa akiwaamrisha kufanya hivyo kama alivyomuamrisha mtu aliyeswali vibaya, kama ilivyoelezwa nyuma.
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiimakinisha mikono yake barabara na magoti yake (kama kwamba akiyashikilia], na alikuwa akivichanua vidole vyake, na alimuamrisha aliyeswali vibaya kama hivyo, kwa kumwambia: *((Utakaporukuu, weka viganja vya mikono yako juu ya magoti yako, na kisha vichanue vidole vyako, kisha bakia (hivyo) hadi kila kiungo kitue mahali pake))* [( Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan katika Swahiyh zao.)].
Alikuwa akijitawanya (sio kujigandamiza mkao mmoja) na akitenganisha viwiko vya mikono na ubavu wake. [( *At-Tirmidhiy ambaye amesema ni Swahiyh, na Ibn Khuzaymah* )]
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anaporukuu, hutandaza mgongo wake na kuusawazisha kiasi kwamba kama ungelimwagiwa maji, basi yangelitua. Na pia alimwambia aliyeswali vibaya: *((Utakaporukuu, weka viwiko vyako juu ya magoti yako, na tawanya mgongo wako na makinisha madhubuti rukuu yako))*.
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) hainamishi kichwa chake wala hakinyanyui (zaidi ya mgongo wake),
bali kilikuwa baina yake. [( *Muslim na Abu 'Awaanah* )]
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/LyNWkET6LdBFjF26pvXS0I
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
*ULAZIMA WA KUTULIA*
*KATIKA RUKUU*
=============♦============
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitulia kwenye rukuu yake, na alimuamrisha awe hivyo aliyeswali vibaya, kama ilivyotajwa katika mlango wa rukuu.
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: *((Kamilisheni rukuu na sujudu, kwani naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hakika mimi nakuoneni nyuma yangu ( Nasema na kuona huku ni kuona kwa uhakika wake kimaumbile, na ni miongoni mwa miujiza yake (صلى الله عليه وآله وسلم), nako ni katika Swalah basi. Na hakuna dalili ya kuona kwa ujumla.) mnaporukuu na mnaposujudu))*.[( Al-Bukhaairy na Muslim )].
Alimuona mtu anaswali bila ya kukamilisha rukuu yake sawa sawa, akidonoa katika sujuud yake, akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): *((Lau atakufa mtu huyu katika hali yake hii, basi atakuwa amekufa katika Mila isiyokuwa ya Muhammad, [anadonoa katika Swalah yake kama adonoavyo kunguru damu]. Mfano wa yule asiyekamilisha rukuu yake na akadonoa katika sujudu yake, ni kama mfano wa mwenye njaa anayekula tende moja au tende mbili, ambazo hazitomfaidisha kitu chochote))* [( Abu Ya'alaa katika Musnad yake (340/3491/1)]
Abu Hurayrah (رضي الله عنه) alisema: *"Rafiki yangu mpenzi (صلى الله عليه وآله وسلم) amenikataza kudonoa katika Swalah yangu mdonowo wa jogoo na kugeuka geuka kama ageukavyo mbweha, na kuchuchumaa kama achuchumaavyo tumbili"* ([ Atw-Twayaalisy, Ahmad na Ibn Abi Shaybah.)] .
Mjumbe wa ALLAAH (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisema: *((Mwizi muovu kabisa miongoni mwa wevi ni yule anayeiba katika Swalah yake))*. Wakasema: *"Ewe Mjumbe wa ALLAAH ! Vipi anaiba katika Swalah yake"*? Akasema: *((Hatimizi rukuu yake na sujuud yake))* ([ Ibn Abi Shaybah (1/89/2),)]
Mara moja, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiswali, na alitupa jicho kwa mtu ambaye hakusawazisha uti wa mgongo wake katika rukuu na sujuud. Alipomaliza alisema: *((Enyi Waislamu! Hakika hakuna Swalah kwa yule asiyesawazisha uti wake wa mgongo katika rukuu na sujuud))*.(( Ibn Abi Shaybah (1/89/2), ))
Akasema katika Hadiyth nyingine: *((Swalah ya mtu haihesabiwi hadi asawazishe mgongo wake katika rukuu na sujuud))* .[( Abu 'Awaanah, Abu Daawuud na As-Sahmiy (61) )]
In Shaa ALLAAH tutaendelea biidhiniLLAAHI
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments